top of page
Rechercher
  • Paul KABUDOGO RUGABA

Ukweli kuhusu kabila la Banyamulenge

Dernière mise à jour : 19 nov. 2020


Mnamo siku hizi, watu wengi hujitokeza na kutapakaza kwenye mitandao ya kijamii maneno machafu kutokana na hisia zao mbovu zenye kujaa fitina, na kuchochea chuki miungoni mwa kabila mbalimbali za jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, hasa kuhamasisha watu kuchukua silaha za aina yote kwa kuua watu wa kabila la wanyamulenge.

Mara wanashuhudiya uwongo hata kutaka kugeuza historia ya nchi ili waweza kuthibitisha kwamba Banyamulenge ni wageni.

Kwa kusaidia vizazi vyetu vinavyo kabilianana na historia mbalimbali za uongo, natoa mchango wangu ili nilete mwangaza.

1. Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika upana wake halisi leo hii, iliundwa na Wazungu wakati mkutano ujulikanao kuwa mkutano wa Berlin uliofanyika nchini u Germani, mnamo mwaka wa 1885. mkutano huu uliitishwa si kwa maslahi ya afrika bali nchi za mabeberu tu. Wakati huo, hakuna mtu Afrika hata mmoja aliyealikwa au aliyehusuria mkutano huo.

2. Mabeberu waligawa Afrika kama ardhi tupu bila kujali taifa zilizokuweko. Hapo mataifa mengi yalijikuta yakigawanywa kati ya inchi mbalimbali, huko mengine tofauti yakiunganishwa kwa kuundwa taifa moja.

3. Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ina pakana na uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Angola, Congo Brazzaville, jamhuri ya Afrika ya kati, na Sudan. Watu wanaoishi karibu na mpaka hupatikana pande zote za mipaka.

4. Ukosefu wa historia kamili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kabla ya ujio wa Wazungu kutoka Ulaya ni shimo kubwa ambayo inasababisha kutapakaza uwongo. Historia za kwanza zilizoandikwa na Wazungu, mara zina makosa. Zimeandikwa bila kujua siku za nyuma, bila kuelewa asili zetu na maana ya mila zetu; kwa nia ya kuwasaidia wao kutawala.

5. Awali namna ya kumiliki ardhi ilikuwa tofauiti kufwatana na desturi na utamaduni wa watu. kulingana na mifumo ya wakati ule hakuwepo mpaka kama iliyvo sasa. Ardhi ilikuwa mali ya kawaida mali ya jamii na ya watu wote. watu walikuwa wakihamahama mara na mara bila kujaza makaratasi au kuonyesha vitambulisho vya aina fulani; kufuatana na sababu nyingi kama hali ya mazingira uchumi, malazi, vita na sababu nyingine:

- Wawindaji walikuwa wakifwata Wanyama, wachugaji vile vile wakiongoza mifugo yao mahali yanaweza kupata malisho na kufanikiwa , wavuvi wakitafuta nafasi watagundua samaki nyingi.

6. Kulikuwa makundi makubwa na madogo . kulingana na idadi ya kabila. makabila makubwa yalikuwa yakiunda ufalme. Mara makabila yalikuwa yakiishi kijirani, mara kama adui.

7. Sekta na kilimo ambyo vinajulikana kuselelesha watu vilikuwa chini ya maendeleo.



8. Utawala wa kikoloni hakutoa fursa sawa kwa wakaaji wote. wale ambao waliweza kushirikiana na utawala kikoloni, walipewa madaraka na kutawala wengine. Wale waliopinga, waliwekwa kando ya utawala na kubaki mbali ya maendeleo. Mfano Wambuti, Banyamulenge, Wanyindu…

9. Ardhi aliyopewa mfalme wa Ubelgiji Leopold II kuwa mali yake binafsi wakati wa mukutano wa Berlin iliitwa nchi huru ya Congo (Etat independent du congo.). Jina la Congo haiamanishi kama wakaaji wa ardhi hiyo wote ni wa kabila ao wa asili ya Kikongo. Wakongo wenyewe wanapatikana katika eneo karibu na bahari ya la Atlantiki. Arthi yawo imegawanywa na kuwa sehemu ya ichi ine ambazo ni Angola, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kongo Brazaville na gabon. Desturi yao ya ki pekee ijulikanayo kua matriarka ( bibi ndiye anajibika na jamaa). Kati ya jamhuri ya kidemokrasi ya congo wanaishi katika mikoa ya Bandundu na Bakongo. Raia wengine wote ni patriarka ( bwana ndiye anajibika na jamaa). Kwa hiyo Mubembe, Mufuliro, Mushi wala Munyamulenge, Munande, Muluba, Mungala,... kwa kitamaduni si Mukongo wa asili hata kamwe bali ni raia wa Congo.

10.Katika nchi huru ya Congo EIC kulikuwepo makundi mbalimbali ambayo sayansi imeainisha kati ya makundi matanu makubwa: wambuti , semi Bantu, Bantu, Hamiti na Nilotiki. Vitabu vingine vinaainisha makundi matatu: wambuti , wa bantu na nilo-hamiti. Kila kundi linaundwa na makundi madogo na vivyo hivyo makundi madogo yana pia mengine madogo zaidi. muundo wa kijamii huonyesha kuwepo kwa kabila (ethnic), kabila (tribe), ukoo (clan), na jamaa. Katika kundi la Nilo-Hamiti ndipo wapo Watutsi na wahima. Katika Watutsi ndipo wapatikanao Banyamulenge wengi


11.Mfalme Leopold II mbele ya kufa , alikabidhi katika urithi inchi huru ya Congo kwa inchi yake ya Ubelgiji. Hapo nchi huru ya Congo ikageuka kama mukoa wa Ubelgiji na ikaitwa Congo Belge.

12.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ni kati ya inchi zilizo badili mara kwa mara utawala na majina. EIC, Congo Belge, Congo, Zaïre, RDC hata Hivyo na taifa lake. Watu pia walibadili majina kulingana na wa Mwelekeo siasa. Majina yote ya ubatizo yalifutwa na kubadilishwa na ya ukoo.

13.Kabila lolote lilikuwa likikaa mipakani mwa ardhi iliyopewa mfalme Leopold II, lina haki yakua na uraia wa Congolese. Banyamulenge walikuwa kati ya ardhi mbele kuundwa kwa Congo kwa hiyo wana kaki kwa uraiya. Hawakuvuka mpaka kwa kuingia inchi ya ugeni. Mpapaka huo ulikuwa bado kuwa. Leo hii kufikiria Banyamulenge kama wahamiaji ni ubaguzi wa kabila tu na kuwaonea.

14.Kabila la wanyamulenge lililo chache linawakilisha "kesi ya kipekee kiutamaduni na kijamii. Banyamulenge Wengi kusema Kinyarwanda kwa lahaja tofauti. Ni wafugaji tangu milenia.

15.Banyamulenge waliishi kijirani na makabila mengine miaka kadhaa bila migogoro. Migogoro yenyewe imeanza na siasa duni zilizo chipuka baada Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kupata uhuru

16.Kuwepo wa Watutsi katika eneo hili ni kwa zamani za kale. Historia ya Kivu, inaonesha wazi ushahidi:

- Pamoja na Banyamulenge, Wami wote wa kabila la bushi wana uhusiano wa kijamii na kiasili ya Watutsi.

- Inajulikana kuwa Bahavu, kabila linaloishi Visiwa vya Ijwi ni mseto wa Watutsi na Bashi

- Burega katika District ya mwenga kuna ukoo miungoni mwa kabila la Warega uitwao Bawanda; asili yake ni Kitutsi.

- Mnamo mwaka 1988 iliandaliwa sherehe baada wabembe kutambua kuwepo miungoni mwao Banyamulenge waliopotelea kwao myaka kadhaa mbele ya ukoloni, nakuweza kuunda jamaa nyingine nyipya kati ya wabembe wajulikanao ni ukoo Bashiluhinda (wabembe) wakiwa ndugu ya ukoo wa Abahinda (wanyamulenge).

17.Bada ya vita vya dunia vya mwaka wa 1914, Ubelgiji ulipewa pia kuongoza Rwanda na Burundi inchi ambazo zilikuwa chini ya utawala wa Ujerumani. Hapo inchi hizo tatu Congo, Rwanda na Burundi ) zilikuwa chini ya utawala moja wa ukoloni wa Ubelgiji. Utawala huo ulichukua watu wengi kutoka Rwanda na Burundi kwenda kufanya kazi Kolwezi (mkoa wa katanga). Hawa walichangana na wazaliwa wa katanga. Hata kama kundi hili ni la asili ya Kitutsi haliitwi Banyamulenge. Watu hawa hujitambua kuwa raia wa Congo. Kwa sababu walihamishwa na utawala uliokuwa na madaraka yote juu ya wananchi wote.

18.Katiba zote hazikubagua Banyamulenge kwani walikua ndani ya masharti yote. Lakini utekelezaji ulionyesha wazi nia mbaya za ubaguzi wa makabila. Historia ya Banyamulenge iligeuzwa mpaka kukanusha uraia wao. Tarehe za kusakinisha zilinyongwa kwa nia ya ukatili.

Ofisini, uraia ulikuwa ukitambuliwa kwa sura.



Sura ya Kitutsi iligeuzwa mara moja sura ya kigeni, na sura ya Kibantu ikawa ndiyo sura ya ki Congomani haizuru iwe mutoka ugenini. sharti ya uchaguzi wa mashindano Miss ilirekebishwa. Hapo kukaundwa dhana ya Miss Bantu ilio weka kikomo kushindana kwa binti Kitutsi kupata tuzo hili. Tayari alikuwa amewekwa mbali. Je hayo yote si ubaguzi ?

19.Kuwa raia jamhuri ya kidemokrasia ya Congo haiamanishi kuwa wa asili ya Kibantu tu. Wa Bantu wote si raia ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, pia raia wote wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo si wa Bantu tu.

20.Baada ya jinamizi la mauaji ya kimbari ya Rwanda, Wahutu walio kimbilia Congo walipewa madaraka ya kunyanyasa na kuua mtu yeyote wa asili ya Kitutsi hasa Banyamulenge, ikisemekana kama Bahutui ni wananchi wenzao wa Congomani na Banyamulenge ni Rwandese wageni .

21.Kuwa Nilo-Hamiti haiamanishi kama sharti kutoka Rwanda ya sasa. Tangu bunia mpaka Kivu ya kaskazini, kuna kabila mbalimbali zenye uhusiano wa kiasili na kundi la Nilo-Hamiti zilikuwa hapo tangu miaka maelfu mbele ya kuundwa kwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, katika hali ya kuhamahama(transhumance).

22.Katiba ya sasa ya kongo inafafanua hadharani kama ardhi ni mali ya serkali. Si mali ya kabila fulani au mtu fulani. Ina uwezo na mamlaka ya kuamua matumizi ya ardhi.

23. Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Ina makabila zaidi ya 450. mila zote na lugha zote zinaruhusiwa bila vikwazo. Hakuna mtu yoyote , ana uwezo wa kuutoa uraia kwa mkaaji, kumuwekea vikwazo kwa utamaduni wake.

24.Banyamulenge walishi kijirani na makabila mengine miaka kadhaa bila migogoro. Walikaa mbali ili kuepuka mifugo yao kuharibu shamba za majirani waliendelea na uhusiano wa kibiashara walibadilishana bidhaa kutoka kwa mifugo na mavuno ya shamba, hapo kabla ya matumizi ya pesa kama ilivyo sasa. Migogoro yenyewe ilizushwa na siasa duni zilizo chipuka baada Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ya kupata uhuru. Kundi la wanamgambo lijukanalo kama simba ndilo limeanza machafuko ya kupora mali, kubaka na kuuwawa kwa watu.

25.Bada ya kushindwa kwa chama hicho cha wanamgambo, serkali haikufanya bidii kuongoa mizizi ya itikadi mbaya ya wanamgambo amboyo ilienda ikageuza sura kutoka kisiasa nakuwa ubaguzi wa kabila. wanasiasa hao walibaki na ndoto ya kulipisha kisasi dhidi ya Banyamulenge kwa kuwa walihusiana na serkali ya Mobutu kwa kulinda usalama wao na mali yao.

26.Serkali katika kutekeleza operesheni zake za kurudisha usalama ndiyo ilitangaza kuwa Fizi ni eneo nyekundu. Lakini kisasi inalipishwa kwa Banyamulenge kwani ni wachache.

27. Walitunga maswali mbalimbali yasiyo na maana na hadisi za uwongo zisizo na msingi kuvutia uhasama dhidi ya Banyamulenge. Hapa tunaweza kutaja.

a. Swali la Dola Hima: ni hadithi bila msingi. Hakuna mtu ya asili ya Banyamulenge aliye fikiria au kua na ndoto ya mradi wa kujenga himaya ya Hima. Hakuna mtu anaweza kutekeleza mradi huo.

b. Swali la kutooana Kati ya Banyamulenge na majirani: Niswali bila msingi. Hakuna sheria ya kimila yeyote inayo mkataza mtu kumuoa mpendwa wake. Na hata sheria hiyo ingelikwa haiwezi kua chanzo cha vita, kwani kila kabila lina wasichana wavulana. Kesi za Watutsi waliooana na kabila nyingine ni nyingi. Kuoana ni swali la kupendana kwa watu wawili. Ikiwa kuna hakufaulu, hio ni kesi fulani binafsi

c. Swali la kutofautisha Banyamulenge na Watutsi wengine wa inchi jirani: Hii ni ubaguzi wenyewe. Banyamulenge wengi walimwa haki zao kwa kisingizio eti wanafana rwandese. Kufanana si kosa. Pia kushindwa kutofautisha sura si swali thabiti. ikiwa utawala ulipeana vitambulisho kwa wale ambao hawana haki ni kosa lake, serkali imeharibika na rushwa. Vitambulisho havikupewa Watutsi tu, watu kutoka kabila mbalimbali za inchi jirani ya cogo walipewa. Haki ni kwamba si jukumu la Banyamulenge na hakuna moja wao aliye husika na kitendo hicho.

d. Swali la kujivunia kabila, utamaduni wao na lugha: Kwangu maoni yangu ni haki ya mtu kupenda , kujivunia na kulinda utamaduni wake, inchi yake. Uzalendo si dhambi.

e. Swali la kugeuza jina la Banyamulenge: si swali thabiti, Kwa maoni yangu, la kusababisha vita. Ni haki ya watu kujiita namna wanavyopenda. Ni kweli kama Banyamulenge walikuwa wakiitwa Wanyarwanda , walitaka jina hilo kugeuka kwa sababu ilikuwa inawapea wanasiasa wabaya fursa kuwaima haki zao na kuwachanganya maoni ya umma juu ya uraia ya kabila hilo. Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ili geuza majina mara kadhaa. Wabembe kwasasa, wanageuza jina bila ubishi wowote na kusema kama wao ni Mmbondo. Kwa nini isiwe hivyo kwa Banyamulenge?

- Serikali haijatamka kamwe hadharani kuhusu uraia wa Banyamulenge, lakini ilionyesha mtazamo wa unafiki kwa kuaacha huru wachochezi wa ubaguzi, kuvumilia mashambulizi mipango michafu kwa lengo la kubagua jamii hili chini ya baraka ya uongozi. Wanao husika katika mipango mibaya, hawajapata hata mara moja tishio la kukatiwa rufaa katika mahakama ao kuwekwa kikorokoroni. Tunaweza kunukuu baadhi ya matukio machache:

- Katibu Yerodia Ndombasi ambaye alialika watu kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Banyamulenge, katika hotuba yake ya uchochezi

- Naibu Gavana wa Sud-Kivu, Lwabanji alisema kuwa katika muda wa siku 7 atafuta Mulenge na Banyamulenge kutoka ramani

- Uvira mkuu wa wilaya, Shweka, alifanya mkutano na maandamano ya kuwinda watu wa asili Banyamulenge.

- Sekatende mpaka sasa anaendelea kutuma vikosi vyake vya mayimayi kushambulia na kupora mali za wa rai Banyamulenge.

- Kizuizi ya kila mara kwa Banayamulenge kuajiri kupiga kura na sensa ya siri navyo pia ni ushahidi lengo hilo.

28.Ni haya kwa inchi kuoana mtu ananyanyaswa kuhusu uraia bada ya miaka maelfu. Inaamanisha ukosefu wa uongozi.

29.Tunaomba jamii ya kistaarabu kuchukua nafasi dhidi tabia kama hiyo ya kuwakandamiza watu.

30. Tunaomba wachochezi kurekebisha dhamiri zao.

31. Ushauri wangu ni huu : ndugu Congolese, Acheni kufuata siasa duni, siasa za akili mbovu na za walioshiba mabaki inchini za mabeberu za kuwaingiza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kuwatumbukiza katika jinamizi la mauaji ya kimakabila. Je namna gani mtu anakwenda Ulaya, Amerika, Canada na pengine pote duniani, baada ya miaka minne anapata neema ya kuwa rai wa inchi iliyompokea, na badaye bila ya kujali , anaendelea kusumbua wananchi walimaliza miaka zaidi ya karne? Je hiyo si ubaguzi mtupu?

32.Dunia hii yageuka ndogo na yazidi kujiunga. Ipo katika ushindani wa maendeleo. Ipo mkononi mwa wanao dhibiti teknolojia na kumiliki mali. Wakaaji wa Kivu kama hawachunguzi vema kwa makini, ardhi hii mnao shuania itachukuliwa na wenye mali toka sehemu zingine.

33.Naalika watu wote wa moyo mwema kujiunga nami kufikiria mambo ya kusaidia na kuleta maendeleo, Kuandika historia kamili ya inchi yetu.

34.Naomba jamii staarabu, umoja wa Afrika, mashirika ya haki za binadamu na watu wote wa moyo mwema kuchukua nafasi kwa kukabiliana na kukomesha ukatili , ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanyiwa dhidi ya Banyamulenge.


Paul Kabudogo Rugaba

23 Aprili 2017

870 vues0 commentaire

Commentaires


bottom of page